Tiago Mendes




Yale magoli mawili ya mwisho, huyu jamaa wa kuitwa Tiago Mendes alihusika nayo yote, moja akitoa pasi ya goli na jengine akifunga mwenyewe kws kupiga chop flani hivi kipa akabaki kuomba heri😂

Wengi hawamfahamu sababu alicheza Chelsea kwa muda mfupi sana, alikuja Chelsea mwaka 2004 akisajiliwa na Jose Mourinho na kuwa mchezaji wa sita kusajiliwa na kocha huyo ambaye alitoka kujiunga na Chelsea akitokea FC Porto alipopata mafanikio na kujulikana zaidi.

Tiago mwenyewe alijiunga na Chelsea akitokea Benfica ya nchini kwao Ureno na alifanya makubwa sana ndani ya kikosi cha Chelsea kilichoshinda ubingwa wa ligi kuu Uingereza na Kombe la Ligi lakini hakudumu, alikuja mwaka 2004 na akaondoka mwaka 2005 mara baada ya Chelsea kumsajili Michael Essien.

Tiago kwasasa ana miaka 42 ndiyo maana hata jana alionekana bado mwepesi na aliubonda fresh kabisa na kwasasa anafanya shughuli ya ukocha.

Comments